

17 March 2025, 12:34 pm
Tarehe 17 ya mwezi Machi 2021 ni siku ambayo Tanzania iliingia simanzi baada ya kifo cha Rais wa awamu ya tano hayati John Pombe Magufuli. Leo imetimia miaka minne tangu kifo chake.
Na: Ester Mabula – Geita
Viongozi mbalimbali wa siasa, dini pamoja na wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini, wameungana kuadhimisha miaka minne ya kifo cha Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli.
Maadhimisho hayo yameongozwa kwa kufanyika ibada maalum ya kumwombea hayati Magufuli katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Yohana Maria Mzeyi lililopo Mlimani wilayani Chato mkoani Geita.