Storm FM

Kanisa Katoliki, GGML wawaibua watoto wenye ulemavu Geita

18 November 2024, 6:16 pm

Picha ya pamoja ya watoto wenye ulemavu wadau wa maendeleo kutoka GGML na viongozi mbalimbali wa kanisa katoliki wakiongozwa Askof wa Jimbo la Geita. Picha na Mrisho Sadick

Katika jamii hususani mikoa ya kanda ya ziwa bado kuna changamoto ya watoto wenye ulemavu kuendelea kufichwa huku imani potofu ikitajwa kuwa sababu.

Na Mrisho Sadick:

Kanisa Katoliki Jimbo la Geita kwa kushirikiana na mgodi wa GGML limefanikiwa kuwaibua watoto wenye ulemavu zaidi ya  5,000 waliyokuwa wamefichwa majumbani katika halmashauri sita za mkoa wa Geita kwa lengo la kuwasaidia kupata haki za msingi ikiwemo elimu.

Askof wa kanisa katoliki jimbo la Geita Flavian Kasala amesema hayo leo Novemba 18,2024 wakati akikabidhi vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika kituo cha shule ya msingi Mbugani nakwamba kanisa hilo kwa kushirikiana na mgodi wa GGML na wadau wengine linatekeleza mradi wa miaka mitatu wa kuondoa imani potofu kuhusu watoto wenye ulemavu kwakuwa idadi kubwa ya watoto hao ukanda wa ziwa wanafichwa majumbani.

Sauti ya Askof Kasala
Askof wa katoliki Jimbo la Geita akimkabidhi vifaa saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mbugani. Picha na Mrisho Sadick

Mratibu wa mradi huo Joseph Masawe amesema mradi huo unatekelezwa katika kata 12 kwenye halmashauri sita za mkoa wa Geita ili kupata takwimu halisi za watoto wenye ulemavu wa kuanzia mwaka 0-12 ili kutambua namna ya kuwasaidia kulingana na ulemavu wao huku diwani wa kata ya Kalangalala Prudence Temba akilipongeza kanisa hilo kwa hatua hiyo.

Sauti ya mratibu wa mradi na Diwani Kalangalala

Kwa upande wake mwakilishi wa mkurugenzi wa Mgodi wa GGML Elibariki Jambau amesema mgodi huo kwa kushirikiana na World Gold Council wamejikita katika kushughulikia changamoto kubwa katika jamii zinazo wakabili watoto wenye ulemavu katika mkoa wa Geita na kwingine.

Sauti ya mwakilishi wa Mkurugenzi wa GGML
Vifaa saidizi mbalimbali vya watoto wenye mahitaji maalumu vyakabidhiwa katika shule ya msingi mbugani. Picha na Mrisho Sadick

Awali akitoa taarifa ya maendeleo ya kituo cha wanafunzi wenye mahitaji maalmu mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mbungani amesema kituo hicho kina wanafunzi 160 nakwamba wengi wao wanaendelea kupata ujuzi mbalimbali huku afisa elimu msingi wa halmashauri ya mji wa Geita Sostenes Mbwilo akilipongeza kanisa katoliki kwa msaada huo.

Sauti mwalimu mkuu na Afisa elimu Geita mji