Jaketi chafu la dereva pikipiki egesho la Mpomvu lachomwa moto
14 November 2024, 10:16 am
Madereva pikipiki mkoa wa Geita wameendelea kusisitizwa kuzingatia usafi hali ambayo inapelekea baadhi ya maegesho kuweka sheria ndogo ndogo ili kuzingatia hilo.
Na: Kale Chongela – Geita
Madereva pikipiki waliopo katika egesho la Mpomvu A kata ya Mtakuja halmashauri ya mji wa Geita wamechoma jaketi la dereva mwenzao ambaye ni mwanachama wa egesho hilo kwa kile walichoeleza kuwa lilikuwa chafu kupitiliza.
Storm Fm ilifika katika mtaa huo kwaajili ya kujiridhisha juu ya kile kilichotokea ambapo yalizuka majibizano kutokana na hatua hiyo iliyochukuliwa.
Baada ya majibizano hayo, baadhi ya wanachama wameeleza sababu hasa zilizopolekea kuchukua uamuzi huo wa kuchoma moto jaketi.
Mwenyekiti wa egesho hilo Bw. Lenard Masele amesema licha ya kuweka makubaliano juu ya usafi pamekuwepo na hali ya baadhi ya wanachama kupuuza agizo hilo na kwamba wameanza kusimamia utaratibu ambao waliuweka katika egesho hilo.
Mwenyekiti wa kata ya Mtakuja Bw Yohana mathias amebainisha kuwa mtumiaji wa jaketi hilo aliwahi kulalamikiwa na abiria kuwa jaketi hilo limekuwa chafu hali ambayo ilikuwa ikisababishwa kutoa harufu mbaya kwa wateja.