Storm FM

Geita yakamilisha maandalizi yote ya mtihani

10 September 2024, 9:19 pm

Mwonekano wa wanafunzi wa shule ya msingi. Picha mtandaoni.

Baada ya kusota kwa miaka saba sasa wanafunzi wa darasa la saba wanakwenda kuhitimu elimu ya msingi kwa kufanya mtihani wa taifa.

Na Eunice Mdui:

Jumla ya watahiniwa 62,489 kutoka shule za msingi 719 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi katika mkoa wa Geita kuanzia Septemba 11 na 12 mwaka huu.

Afisa Elimu Mkoa wa Geita Anthony Mtweve akizungumza na Storm FM hii leo amesema serikali imekamilisha maandalizi yote muhimu kwa ajili ya mtihani wa taifa nakuwataka wazazi na walezi kuwajibika kwa watoto wao huku akiwaonya baadhi ya watu waliopanga kufanya udanganyifu kwenye mtihani huo

Sauti ya Afisa Elimu mkoa wa Geita

Kati ya watahiniwa hao 62,489 wavulana ni 28,600 na wasichana 33,889.

Watahiniwa 1,230,780 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi nchini (PSLE) huku Baraza la Mtihani Tanzania(NECTA) likiwatahadharisha kuwafutia matokeo watakaobanika kufanya udanganyifu.