Wakulima wa Alizeti Geita mjini wapigwa msasa
2 September 2024, 1:58 pm
Safina ya idara ya vijana imeendelea kutoa mafunzo na elimu kwa makundi mbalimbali ya watu ili kuwasaidia kujikwamua katika shughuli zao za kiuchumi.
Na: Kale Chongela – Geita
Ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita kwa kushirikiana na uongozi wa Safina idara ya vijana na shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO mkoa wa Geita wametoa mafunzo ya siku 2 kwa wakulima wa zao la Alizeti kutoka halmashauri ya mji wa Geita.
Afisa kilimo kutoka halmashauri ya mji wa Geita Bi. Roza William amesema kuwa lengo la kutoa elimu na mafunzo hayo ni kuongeza idadi kubwa ya wakulima wa zao hilo.
Mafunzo hayo yamefanyika katika kiwanda cha kuchakata alizeti cha Safina idara ya vijana ambapo afisa kutoka SIDO mkoa wa Geita Bw. Daudi Kioleri amesema jukumu kubwa ni kuendelea kutoa maarifa kwa wananchi ili kujikwamua kiuchumi kupitia viwanda vidogo vidogo
Baadhi ya wakulima ambao wameshiriki semina hiyo wameahidi kutumia vyema ujuzi ambao wamepewa na watalaamu hao ili kuongeza tija zaidi.
Makamu wa Askofu kanisa la AICT ambao ndiyo wasimamizi wakuu wa Safina idara ya vijana Dayosisi ya Geita Mchugaji Obed Nkulukulu amesema jukumu lao kubwa ni kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi