Mtetezi wa mama Chato kusimama na Rais Samia uchaguzi serikali za mitaa
19 January 2024, 12:54 pm
Baadhi ya vijana wilayani Chato wameonesha hisia zao kwa kuungana na Rais Dkt Samia kwa kile walichokieleza kuwa wana imani na serikali yake.
Na Daniel Magwina:
Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi Mkuu mwaka 2025 vijana wilayani Chato Mkoani Geita wameahidi kumuunga Mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwakuwa amefanya kazi kubwa kwa kipindi kifupi kwenye utawala wake.
Vijana hao Kutoka Taasisi ya Mtetezi wa Mama wilayani Chato Mkoani Geita wakiwa kwenye Kata ya Bwanga wilayani humo wamesema hakuna sababu ya kuwaondoa viongozi wa CCM huku wakiahidi kusimama na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwakuwa amefanya kazi kubwa ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo kuendelea kutoa fedha za kukamilisha ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Kanda Chato.
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Mkoa wa Geita Emmanuel Mgeta amesema wamekubaliana kwa pamoja kumuunga Mkono Rais Dkt Samia pamoja na kutangaza mazuri yake.