Storm FM

Wananchi Geita wahimizwa kuhakiki mizani kabla ya kununua

10 October 2024, 11:57 am

Kaimu meneja wa wakala wa vipimo mkoani Geita akizungumza na Storm FM. Picha na Ester Mabula

Wakala wa vipimo nchini Tanzania wameendelea kutoa elimu juu ya vipimo sahihi kwa wananchi na wafanyabiashara ili kuondoa changamoto mbalimbali.

Na: Ester Mabula – Geita

Kaimu meneja wa wakala wa vipimo mkoa wa Geita amesema kwa sasa wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi katika maonesho ya 7 ya teknnolojia ya madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZA Bombambili mjini Geita hivyo amewahimiza wananchi kufika katika banda lao ili kupata elimu zaidi.

Sauti ya kaimu meneja

Ameeleza kuwa ni muhimu mfanyabiashara au mwananchi anayetaka kuanza biashara kuhakiki mzani anaonunua uwe na nembo ambayo imehakikiwa ili kuondoa changamoto na migongano inayoweza kujitokeza.

Sauti ya kaimu meneja
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika banda la wakala wa vipimo Tanzania mkoa wa Geita ili kupata elimu. Picha na Ester Mabula

Katika hatua nyingine amewasihi wananchi wanaopima uzito kwa watu wanopita mtaani kujiridhisha na mizani wanayotumia ili kupata majibu sahihi.

Sauti ya kaimu meneja

Maonesho ya 7 ya teknlojia ya madini yanaendelea mkoani Geita ambapo yalianza Oktoba 02, 2024 na yanatarajiwa kufungwa Oktoba 13, 2024 amabapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika banda la wakala wa vipimo Tanzania mkoa wa Geita ili kupata elimu. Picha na Ester Mabula