Washindi Dimbani Cup shangwe tu
15 August 2023, 1:55 pm
Wadau wa soka Mkoani Geita wameendelea kuzipongeza taasisi za umma na binafsi kwa kuendelea kuuthamini mchezo wa mpira wa miguu kwa kuandaa mashindano mbaimbali ambayo yamekuwa chachu kwa kuibua vipaji vya vijana.
Na Amon Bebe – Geita
Baada ya fainali ya michuano ya Mpira wa Miguu inayojulikana Dimbani Cup, ambayo huandaliwa na Storm FM na kumalizika jana katika uwanja wa shule ya Sekondari Kalangalala, huku Bingwa akiwa Geita All Stars na nafasi ya pili ni Geita Veterani na kukabidhiwa zawadi ya pesa taslim shilingi laki sita huku mshindi wa pili Geita Veteran akipata shilingi laki nne.
Wanafainali hao pia wamekabidhiwa mipira miwili kwa mshindi wa kwanza na mmoja kwa mshindi wa pili na Diwani wa Kata ya Kalangalala Pludence Temba, kwa niaba ya Mbunge wa Geita mjini Constantine Kanyasu ikiwa ni ahadi aliyotoa kwenye fainali hapo Jana kuwaunga mkono Storm FM kwa kuongezea zawadi za washindi.
Mhe Temba ameipongeza Storm FM kwa kuendeleza michezo hapa mkoani Geita ikiwa ni pamoja na kusaidia jamii katika mambo mbalimbali.