Storm FM

CCM yazindua jengo la kitega uchumi Jumuiya ya wazazi Geita

15 January 2025, 10:57 am

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya utekelezaji wa Jumuiya ya wazazi (CCM) mkoa wa Geita. Picha na Nicholaus Lyakando

Watumishi wa  Umoja wa Jumuiya wa wazazi kupitia chama cha mapinduzi (CCM mkoa wa Geita  wametakiwa kutunza na Kulinda Nyumba za Jumuiya hiyo na wala wasigeuze Matumizi yake.

Na: Nicholaus Lyankando – Geita

Wakizungumza katika uzinduzi wa Jengo jipya  la kitega uchumi la Jumuiya hiyo lililopo katika mtaa wa Magogo litakalo gharimu kiasi cha shilingi milioni 55, baadhi ya wenyeviti wa Jumuiya kutoka wilaya za Geita wameonya kuhusiana na matumizi mabaya ya nyumba hizo huku wakieleza mikakati ya kukamilisha maboma yaliyosalia.

Sauti ya wenyeviti

Katibu wa Jumuiya wa wazazi mkoa wa Geita Bwana Philibet Ngemela ametaja thamani ya nyumba iliyokamilika ya katibu wa mkoa huku akieleza azma ya kuwa na majengo hayo ni pamoja na kuondokana na hali upangaji katika majengo ya watu binafsi.

Sauti ya Katibu
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Geita Lukas Mazinzi. Picha na Nicholaus Lyankando

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Geita Lukas Mazinzi amesema kufikia mwezi April mwaka huu watakuwa wamekamilisha maboma yote huku akitoa maagizo kwa wenyeviti wa wilaya kuwa waaminifu katika matumizi ya fedha za mradi.

Sauti ya mwenyekiti

Baada ya kukamilisha zoezi la uzinduzi nakuzitembelea Nyumba hizo za watumishi Jumuia hiyo walifanya Kikao cha kutathimini Shughuli zote zilizofanyika kutoka Mwaka jana hadi mwaka Huu