Wapata ajali wakisafirisha maiti kwa bodaboda kutoka Geita-Kagera
8 January 2025, 3:51 pm
Waendesha pikipiki wanne wa egesho la Miti mirefu mtaa wa Mission mjini Geita wamenusurika kifo baada ya kupata ajali walipokuwa wakisafirisha jeneza lenye maiti ndani yake kutoka Geita kuelekea Bukoba kwaajili ya mazishi.
Na: Amon Mwakalobo – Geita
Tukio hilo limetokea Januari 05, 2025 majira ya saa tano usiku baada ya kuwasili Muleba Bukoba KM chache kabla ya kufika nyumbani kwao na Marehemu.
Akisimulia tukio hilo dereva wa pikipiki iliyobeba jeneza na wenzake wamesema ajali hiyo iimetokea baada ya pikipiki ya mbele ambayo ilibeba maiti kusimama ghafla na kupelekea zilizokuwa nyuma yake kuingia mtaroni wakiogopa kugonga jeneza.
Baadhi ya maderva pikipiki wameeleza juu ya tukio hilo na kusema kuwa ni kutokana na ukaribu waliokuwa nao pamoja na marehemu na hivyo hilo jambo limefanyika kwa upendo.
Kwa upande wa baadhi ya wananchi kutoka mjini Geita wameshangazwa na kitendo cha bodaboda kubeba maiti huku wakishauri mamlaka husika kuingilia kati.
Kwa upande wake mkaguzi msaidizi wa polisi kitengo cha usalama barabarani afande Mark Thomas Masawe kutoka mkoani Kagera amesema Jeshi la polisi hawashauri kufanya hivyo.