Storm FM

Katibu ACT Wazalendo ziarani wilayani Mbogwe

30 September 2024, 5:31 pm

Katibu mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu Ado akizungumza na wananchi wilayani Mbogwe mkoani Geita.

Chama cha ACT Wazalendo kimeendelea na ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali nchini ambapo awamu hii wanaendelea na ziara katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Na: Ester Mabula – Geita

Katibu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu Ado Septemba 29, 2024 akiwa wilayani Mbogwe mkoani Geita katika iara yake ameitaka serikali kuweka mazingira rafiki kwa wakulima kupata mbolea za ruzuku kwa wakati na kuondoa janja janja ya kunufaisha watu wachache kwa maslahi yao binafsi.

Sauti ya Katibu ACT Wazalendo
Wananchi wa kijiji cha Mbongwe wakimsikiliza katibu mkuu wa ACT Wazalendo katika mkutano wa hadhara.

Aidha amesema kuwa mpango wa kunusuru kaya maskini wa TASAF unatakiwa kuwanufaisha walengwa na wanufaika na si vinginevyo.

Sauti ya Katibu wa ACT Wazalendo
Wananchi wilayani Mbogwe wakifuatilia mkutano wa katibu mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu Ado.

Ziara ya Katibu mkuu wa ACT Wazalendo kwa mikoa ya kanda ya ziwa ilianza Septemba 20, 2024 ambapo ametembelea mikoa ya Simiyu, Mara, Mwanza, Geita na itamalizika mkoani Kagera.