Storm FM

Mnyama Kiboko aliyesumbua kwa miaka 5 auawa Geita

23 January 2025, 4:21 pm

Wananchi wa kijiji cha Itale wakiwa wamemzuguka Kiboko baada ya kuuawa. Picha na Edga Rwenduru

“Tunaishukuru serikali kwa kuweza kumuua mnyama huyu maana ilikuwa ni changamoto kubwa tukiishi kwa uoga”- mwananchi Itale

Na: Edga Rwenduru – Geita

Mnyama Kiboko aliyekuwa anaua mifugo na kuharibu mazao ya wananchi wa kijiji cha Itale kata ya Katoma halmashauri ya wilaya ya Geita ameuawa na Askari wa mamlaka ya usimamizi wa wanayamapori Tanzania TAWA usiku wa kuamkia Januari 22 mwaka huu.

Wananchi wa kijiji hicho wametoa shukrani kwa mamlaka ya wanyamapori Tanzania (TAWA) kwa kuchukua uamuzi wa kumuua kiboko huyo kwani wakazi wa kijiji hicho walikuwa wanaishi kwa hofu kubwa.

Sauti ya wananchi
Wananchi wakianza zoezi la kumchuna ngozi kwaajili ya kugawana vitoweo. Picha na Edga Rwenduru

Josephat Komanya ni diwani wa kata ya Katoma amesema kuwa wakazi wa kijiji hicho sasa wamepata amani kwani mnyama huyo aliua ng’ombe watatu na kuharibu mazao huku akiiomba serikali na TAWA wadhibiti pia Mamba ambao ni tishio kwa maisha ya wakazi hao.

Sauti ya diwani Josephat Komanya

Kwa mujibu wa mwakilishi wa Kamanda wa TAWA kanda ya ziwa Afisa wanyamapori msaidizi daraja la pili Sefu Marambo amesema hatua hiyo imekuja kufuatia barua waliyoipokea kutoka halmashauri ya wilaya ya Geita ikiwataka kumdhibiti Mnyama huyo.

Sauti ya mwakilishi wa kamanda wa TAMWA
Wananchi wakiendelea na zoezi la kumchuna ngozi Kiboko. Picha na Edga Rwenduru