Storm FM

Zifahamu fursa za Geita kuwa Manispaa

15 January 2025, 11:08 am

Mstahiki Meya wa manispaa ya Geita Costantine Morandi akiwa katika studio za Storm FM

Disemba 13, 2024 waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa alitoa taarifa ya kupandisha hadhi halmashauri ya mji wa Geita kuwa manispaa.

Na: Ester Mabula – Geita

Mstahiki meya wa manispaa ya Geita Costantine Morandi amesema kuwa imekuwa neema kwa halmashauri ya mji wa Geita kupanda hadhi na kuwa manispaa kwani itasaidia katika kuongeza juhudi za kimaendeleo kwa ujumla.

Ameeleza hayo akiwa katika kipindi cha Storm Asubuhi leo Januari 15, 2025 na kubainisha fursa ambazo zitapatikana kutokana na hatua hiyo.

Sauti ya mstahiki Meya Costantine Morandi

Akibainisha juu ya uboreshaji wa miundombinu ya Geita ameeleza juu ya mradi wa barabara unaoendelea wa KM 17 wenye lengo la kuboresha na kuondoa changamoto ya baadhi ya barabara.

Sauti ya mstahiki Meya Costantine Morandi