Wafanyabiashara soko la Lwamgasa watoa ombi kwa Serikali
13 December 2024, 12:04 pm
Lwamgasa ni miongoni mwa kata 37 zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Geita ambapo shughuli kuu inayofanyika katika kata hiyo ni uchimbaji wa madini ya dhahabu.
Na: Paul William – Geita
Wafanyabiashara mbalimbali katika soko kuu la kata ya Lwamgasa wilayani na mkoani Geita wameiomba serikali kuwasaidia kuboresha soko hilo kutokana na kuzidiwa na idadi ya watu wanaofika hapo kwaajili ya kupata huduma
Wakizungumza na Storm FM Disemba 13, 2024 wamesema endapo soko hilo litaboreshwa itasaidia kuweza kuongeza mapato na kutoa wigo mpana kwa wao kufanya biashara pasipo kulundikana kwani kwa sasa linazidiwa na watu.
Akizungumzia suala hilo mjumbe wa serikali ya mtaa Bwana Fredrick Jeremia Wambowe amesema kwa kuwa wamechaguliwa na wananchi katika kitongoji hicho ambapo soko hilo linapatikana watahakikisha soko hilo linaboreshwa.
Wakingumzia hali ya kibiashara katika soko hilo kwa sasa katika msimu huu wa mwisho wa mwaka, wafanyabiashara wamesema hali ya kimauzo inabadilika badilika.