Storm FM

Maambukizi ya VVU yapungua mkoa wa Geita

3 December 2024, 12:43 pm

Mratibu wa VVU mkoa wa Geita Dkt. Yohanne Kihaga atitoa taarifa ya hali ya maambukizi mkoa wa Geita. Picha Kale Chongela

Siku ya UKIMWI duniani huadhimishwa kila Disemba 01, kila mwaka ili kuhamasisha watu umuhimu wa kupima, kujikinga, na kutoa msaada kwa watu wanaoishi na maambukizi ya VVU.

Na: Kale Chongela – Geita

Hali ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI mkoa wa Geita imepungua kwa asilimia 0.1 kutoka asilimia 5 hadi asilimia 4.9 huku kundi la wanaume likitajwa kuongoza kwa maambukizi.

Takwimu hizo zimetolewa na mratibu wa VVU mkoa wa Geita Dkt. Yohanne Kihaga wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI Disemba mosi, ambayo kimkoa yalifanyika katika kata ya Bukwimba wilayani Nyang’hwale ambapo amesema mkoa wa Geita una makadirio ya watu 95,100 wanaoishi na maambulizi ya VVU na kati yao asilimia 73.1 wanatambua hali zao za maambukizi.

Sauti ya mratibu VVU mkoa wa Geita
Wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyoadhimishwa kata ya Bukwimba. Picha na Kale Chongela

Mjumbe wa kamata ya  utetezi wa watu wenye VVUhalmashauri ya mji wa Geita Bw. Ponsian Stanslaus ametumia fursa hiyo kusihi jamii kuachana na dhana potofu za kuwatenga watu wenye VVU.

Sauti ya Ponsian Stanslaus

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Geita, mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba amewataka watendaji wa serikali na wadau wa mapambano dhidi ya VVU mkoani Geita kuendelea kuwawezesha kiuchumi watu wanaoishi na maambukizi pamoja na kutekeleza afua na sera mbalimbali za mapambano dhidi ya VVU.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Geita