Storm FM

Rais Samia atoa tuzo kwa GGML ushiriki bora wa maonesho Geita

14 October 2024, 10:49 am

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu akikabidhi tuzo kwa makamu wa Rais mwandamizi wa Anglo Gold Ashant Terry Strong.

Oktoba 13, 2024 yamehitimishwa rasmi maonesho ya 7 ya teknolojia na uwekezaji katika sekta ya madini ambayo yalikuwa yakiendelea katika viwanja vya EPZA mjini Geita tangu Oktoba 02, 2024.

Na: Ester Mabula – Geita

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekabidhi tuzo kwa kampuni ya uchimbaji madini ya Geita Gold Minning Limited (GGML) ikiwa ni sehemu ya kutambua ushiriki wake bora na udhamini wake mkuu katika maonesho ya teknolojia na uwekezaji katika sekta ya madini ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka mkoani Geita.

Wananchi kutoka maeneo mbalimbali waliojitokeza katika kilele cha maonesho ya teknolojia ya madini

Tuzo hiyo imepokelewa na makamu wa Rais mwandamizi wa Anglo Gold Ashanti Afrika, Terry Strong ambaye amesema GGML itaendelea kuwezesha miradi mbalimbali kupitia CSR ambapo kila mwaka hutenga shilingi bilioni 9 kwaajili ya miradi hiyo sambamba na kuboresha elimu, miundombinu, afya na miradi mingine ya maendeleo.

Rais Samia ameelezea mkakati wa serikali kuongeza wastani wa upimaji maeneo palipo na dalili za upatikanaji wa madini.

Sauti ya Rais SSH

Wakizungumzia maonesho hayo, baadhi ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali nadni na nje ya mkoa wa Geita wameeleza manufaa ya maonesho hayo kiuchumi

Sauti za wananchi