Storm FM

Kiongozi mbio za mwenge aridhishwa na mradi wa maji Mbogwe

3 October 2024, 9:43 am

Mradi wa maji unaotarajiwa kukamilika April, 2025 ambao utanufaisha wakazi na wananchi wa wilaya ya Mbogwe. Picha na Kale Chongela

Mwenge wa uhuru umeendelea kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Geita tangu ulipokabidhiwa rasmi Septemba 30, 2024.

Na: Kale Chongela – Geita

Mbio za Mwenge wa uhuru zimeridhishwa na mradi wa maji wenye thamani ya 2,050,923,546.11 uliopo wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.

Mhandisi kutoka RUWASA Rodrick Mbepera akikinga maji katika mradi unaoendelea kujengwa wilayani Mbongwe. Picha na Kale Chongela

Akitoa taarifa mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Oktoba 02, 2024 mhandisi wa wakala wa maji vijijini (RUWASA) wilaya ya Mbogwe Mhandisi Rodrick Mbepera amesema mradi huo unatarajia kukamilika mwezi April, 2025.

Sauti ya mhandisi kutoka RUWASA

Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wameishukuru serikali kwa ujenzi wa mradi huo wa maji kwani utawasaidia kuondoa changamoto ya muda mrefu kutokana na kusogezewa karibu huduma ya maji.

Sauti ya wananchi

Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Ndugu Godfrey Mzava ameweka njiwe la msingi katika mradi huo wa maji wenye tenki la ujazo wa lita laki moja na elfu hamisini.

Sauti ya Godfrey Mzava
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Godfrey Mzava akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa maji Mbogwe