GGML yaanza maandalizi ya Kili challenge 2024
8 July 2024, 10:07 am
Kampeni ya Kili challenge huratibiwa na mgodi wa dhahabu wa Geita Gold mine limited (GGML) kwa kushirikiana na tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) ambapo hufanyika Julai ya kila mwaka.
Na: Kale Chongela – Geita
Uongozi wa mgodi wa Geita Gold Mine Limited (GGML) umefanya hamasa kwa wananchi wa wilaya ya Chato mkoani Geita kwa lengo la kushirikiana kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Julai 19 mwaka huu.
Akizunguza na waandishi wa habari Julai 06, 2024 baada ya usafi wa mazingira sambamba na zoezi la upandaji miti katika hospitali ya wilaya ya Chato, meneja mahusiano wa GGML Bw. Gilbert Moria amesema kwa mwaka huu wanatarajia kuwa na wapanda mlima 70.
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Chato Dkt. Herieth Majaliwa ametumia fursa hiyo kuushukuru uongozi wa GGML kushiriki kufanya usafi sambamba na kupanda miti katika eneo hilo.
Kwa upande wake meneja wa afya, usalama na mazingira wa GGML Dkt. Kiva Mvungi amesema fedha ambazo zinapatikana kutokana na zoezi la upandaji mlima kilimanjaro husaidia mapambano dhidi ya UKIMWI hapa nchini na kwamba wanatarajia kukusanya bilioni 2.6.