TCRA Kanda ya Ziwa yawapiga msasa waandishi wa habari Geita
5 June 2024, 11:29 am
TCRA kanda ya ziwa imeendelea kutembelea mikoa ya ukanda huo na kutoa elimu kwa waandishi wa habari kuendelea kuzingatia miiko ya habari na weledi katika kutoa taarifa.
Na: Kale Chongela – Geita
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imewataka waandishi wa habari kuwasilisha maudhui yenye tija kwa jamii ili kuondokana na taarifa za upotoshaji ambazo zinaweza kuleta taharuki kwa jamii.
Kauli hiyo imetolewa na Meneja wa TCRA kanda ya ziwa mhandisi Imelda Salum baada ya semina iliyokutanisha waandishi wa habari na maafisa habari mkoani Geita iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita ambapo amefafanua kuwa kalamu za waandisi zisiwe chanzo cha upotoshaji kwenye jamii.
Baadhi ya waandishi wa habari ambao wameshiriki semina hiyo wameahidi kuendelea kuzingatia maelekezo ambayo yamekuwa yakitolewa na TCRA.
Mamlaka ya mawasiliano nchini imeedelea kusimamia vyombo vya habari na kwa kuelekeza waandishi wa habari kuzingatia maudhui yeye tija ili kusaidia kuondoa upotoshaji wa taarifa.