Magonjwa yasiyo ya kuambukiza tishio wilayani Geita
18 November 2023, 3:38 pm
Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yameendelea kuwa tatizo miongoni mwa wakazi wa Mkoa wa Geita huku mtindo wa maisha ukitajwa kuwa sababu.
Na Mrisho Sadick – Geita
Idadi ya wagonjwa wanaosumbuliwa na Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ikiwemo kisukari katika kituo cha Afya Kasamwa wilayani Geita inazidi kuongezeka kutokana na wananchi kubadili mtindo wa maisha hususani kwenye upande wa chakula.
Mganga Mfawidhi wa kituo hicho anasema maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanawasha taa kwa wananchi kutambua uwepo wa tatizo hilo huku wadau wa maendeleo ikiwemo taasisi ya Mtetezi wa mama wakiendelea kuikumbusha Jamii umuhimu wa kupima Afya zao mara kwa mara.
Mwenyekiti wa taasisi ya Mtetezi wa mama katika Halmashauri ya mji wa Geita Agatha Kyusa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma za afya nakuwataka wananchi kutambua umuhimu wa kupima afya zao hususani magonjwa yasiyoyakuambukiza.
Katibu wa Taasisi hiyo Rahma Yusufu na Mjumbe Hassan Suleiman wamesema Katika maadhimisho hayo ya wiki ya magonjwa yasiyoyakuambukiza taasisi hiyo ikiwa katika kituo cha afya Kasamwa imepima Afya , imechangia damu , imefanya usafi , imepanda miti nakutembelea wagonjwa nakuwataka wananchi kuendelea kujenga tabia ya kufika Hospitali pindi wanapokabiliwa na Changamoto za kiafya.
Maadhimisho haya yanaongozwa na Kaulimbiu isemayo “Usijisahau Jali Afya yako”