Madereva Geita waonywa kutii sheria za barabarani
9 December 2024, 3:40 pm
Jeshi la polisi nchini kitengo cha usalama barabarani limeendelea kujiimarisha kwa kufanya ukaguzi kwa madereva na vyombo vya moto ili kubaini makosa mbalimbali na kuyachukulia hatua.
Na: Kale Chongela – Geita
Jeshi la Polisi kitengo cha usalama Barabarani nchini limewaonya baadhi ya madereva na mawakala wa magari ya abiria kuacha tabia ya kupandisha nauli katika sikukuu za mwisho wa mwaka kinyume na utaratibu.
Onyo hilo limetolewa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani nchini Naibu Kamishna wa polisi (DCP) Ramadhani Ng’azi akiwa katika kituo kikuu cha mabasi ya abiria mkoani Geita wakati wa zoezi la ukaguzi wa magari ya abiria ikiwemo kuwapima vilevi madereva ikiwa ni mwendelezo wa kukabiliana na ajali za barabarani.
Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Geita Aloyce Jacob amewataka madereva kufuata sheria ili kuepuka kuingia mikononi mwa Jeshi hilo.
Kwa upande wake Afisa leseni kutoka mamlaka ya udhibiti wa usafiri nchi kavu (LATRA) mkoa wa Geita Kenani Katindasa amesema wataendelea kusimamia sheria za ukataji tiketi kwa abiria.