Wivu wa mapenzi wapelekea nyumba kuchomwa moto Mgusu
5 December 2024, 9:48 am
Wivu wa mapenzi umeendelea kutajwa kuwa chanzo cha migogoro ya kifamilia ambayo inapelekea madhara mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mali.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Nyumba ya Michael Joseph Nzumbi mkazi wa mtaa wa Mgusu kata ya Mgusu wilayani na mkoani Geita imechomwa moto na mwanamke anaedaiwa kuwa ni mke wake huku chanzo cha tukio hilo kikiwa ni wivu wa kimapenzi
Tukio hilo limetokea Disemba 01, 2024 majira ya asubuhi wakati Michael Nzumbi akiwa kanisani ambapo alipigiwa simu na kupewa taarifa juu ya tukio hilo.
Akiendelea kuzungumzia tukio hilo ameiomba serikali na Jeshi la polisi kuchukua hatua za haraka kwa watu wanaokwamisha maendeleo kwa kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani.
Baadhi ya mashuhuda ambao ni majirani zake walioshiriki katika zoezi la kuzima moto na kuokoa baadhi ya mali, wameeleza kusikitishwa na tukio hilo ambapo wamefafanua namna lilivyoweza kujitokeza.
Viongozi wa eneo hilo akiwemo Balozi na Mwenyekiti wa mtaa wa mgusu, Emmanuel Mapalala walikuwa na haya ya kuelezea.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Geita SACP Safia Jongo amesema taarifa za tukio hilo zimefika ofisini kwake ambapo taratibu nyingine za ufatiaji zaidi zikiendelea.