Storm FM

Aliyeua kwenye fumanizi ashikiliwa na polisi Geita

7 November 2024, 4:42 pm

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo akizungumza na waandishi wa habari. Picha na Evance Mlyakado

Jamii mkoani Geita imeendelea kukumbushwa kuacha kujichukulia sheria mkononi ili kuepusha madhara yanayojitokeza ikiwemo vifo vya baadhi ya watu.

Na: Evance Mlyakado – Geita

Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kukamatwa kwa Athuman Baseka (39) fundi seremala mkazi wa Kamhanga wilayani Geita kwa kwa tuhuma za mauaji ya Faida Deus (34) mkazi wa kitongoji cha Mwamashiki kijiji na kata ya Bugarama na kuongeza kuwa taratibu za uchunguzi zikikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Sauti ya Kamanda
Jesca Emmanuel, mke wa marehemu Faida Deus aliyeuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali. Picha na Evance Mlyakado

Kwa upande wake mke wa marehemu Bi. Jesca Emmanuel ameeeleza jinsi walivyokuwa wakiishi na mume wake kabla ya umauti.

Sauti ya mke wa marehemu

Baba wa marehemu Deus Lubitila Masalu ameiomba serikali kumchukulia hatua stahiki mtuhumiwa wa mauaji ya mtoto wake ili kukomesha vitendo vya namna hiyo kwenye jamii.

Sauti ya baba mzazi wa marehemu

Kijana Faida Deus (34) aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake huku chanzo cha mauaji hayo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi katika tukio lililotokea usiku wa Oktoba 30, 2024 katika kijiji cha Bugalama wilayani na mkoani Geita.

Kaburi la Faida Deus baada ya kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele. Picha na Evance Mlyakado