Storm FM
Wakimbiza Baiskeli (Daladala) Washauriwa Kutumia Lugha Za Staha.
31 May 2021, 7:51 pm
Na Zubeda Handrish:
Waendesha Baiskeli maarufu kwa jina la (Daladala) Mkoani Geita wamewashauriwa kutumia lugha za staha na kuzingatia suala la usafi na utunzaji wa mazingira wawapo katika vituo au vijiwe vyao vya kazi
Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Msalala Road Bwana Sostenes Karist alipozungumza na Storm FM mara baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa moja ya mwananchi wake juu ya Daladala hao kutumia lugha za matusi na kuchafua mazingira katika eneo wanapoegesha baiskeli zao
Nao waendesha baiskeli wanaofanya shughuli zao katika mtaa huo wamekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kuahidi kubadilika ili kufanya shughuli zao kwa amani na kwa kufuata utaratibu wa mtaa huo.