Storm FM

Ezy Auto Motors yakabidhi gari kwa mteja aliyeagiza mkoani Geita

12 October 2024, 10:22 am

Banda la Ezy Auto motors katika maonesho ya 7 ya teknolojia ya madini viwanja vya EPZA mjini Geita.

Wakazi wa Geita hatimaye wamefikiwa na kurahisishiwa kuagiza magari kwa usalama na uhakika zaidi kwa mpango wa kuwekeza, mkopo au kulipa moja kwa moja.

Na: Ester Mabula – Geita

Katika hafla iliyojaa furaha, kampuni maarufu ya uuzaji magari nchini Ezy Auto Motors yenye matawi katika mikoa ya Dar es salaa, Dodoma, Mwanza na Geita, Oktoba 11, 2024 ilikabidhi gari jipya kwa mteja wake, Bi. Ruth Keto mkazi wa mtaa wa Mwatulole mjini Geita ambaye aliagiza gari hilo kwa njia ya mtandao.

Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi za Ezy Auto motors zilizopo eneo la soko la dhahabu mjini Geita ambapo mteja alionyesha furaha kubwa baada ya kupokea gari lake likiwa salama.

Sauti ya mteja
Afisa msimamizi Yona Asheri Nasania akikabidhi hati ya gari kwa Ruth Keto mara baada ya makabidhiano ya gari.

Bi. Ruth ambaye ni mfanya kazi katika taasisi ya kifedha (Benki) alielezea kuridhishwa kwake na huduma aliyopata kutoka Ezy Auto motors, “Nimekuwa nikifuatilia kampuni hii kwa muda mrefu, na leo nashuhudia ukweli wa ahadi zao za uaminifu na ubora,” alisema.

Afisa msimamizi wa kampuni hiyo kanda ya ziwa Bw. Yona Asheri Nasania amesisitiza umuhimu wa kujenga uhusiano mzuri na wateja akisema wanaamini katika kutoa huduma bora na za uaminifu.

Sauti ya Afisa msimamizi

Kwa sasa Ezy Auto motors wapo katika maonesho ya 7 ya teknolojia ya madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZA Bombambili mjini Geita ambapo wameendelea kutoa huduma kwa wnaanchi.

Bi. Ruth Keto na Afisa msimamizi Yona Asheri wakiwa mbele ya gari aliloagiza na Ezy Auto Motors katika hafla ya makabidhiano

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma na magari yanayopatikana, tembelea tovuti rasmi ya Ezy Auto motors (www.ezy.co.tz) au wasiliana nao kupitia mitandao yao ya kijamii.