Storm FM

Dkt. Biteko ahimiza wananchi Geita kujiandikisha

11 October 2024, 12:25 pm

Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Dkt. Doto Biteko akijiandikisha katika daftari la mpiga kura. Picha na Mrisho Sadick

Leo Oktoba 11, 2024 limezinduliwa rasmi zoezi la kujiandikisha katika daftari la mpiga kura kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.

Na: Mrisho Sadick – Geita

Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Dkt. Doto Mashaka Biteko amewataka wakazi wa wilaya ya Bukombe mkoani Geita kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wakazi kwa ajili ya kupata nafasi ya kuchagua viongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Naibu waziri mkuu Dkt. Doto Biteko akiwa katika foleni pamoja na wananchi kwaajili ya kujiandikisha katika daftari la makazi wilayani Bukombe. Picha na Mrisho Sadick

Dkt. Biteko ametoa kauli hiyo baada ya kumaliza kujiandikisha katika daftari la mkazi katika kituo cha Bulangwa wilayani Bukombe mkoani Geita huku akiwataka wananchi kutosubiri hadi siku ya mwisho na badala yake wajitokeze kwa wingi kujiandikisha ili wapate haki yao ya msingi ya kupiga kura.

Sauti ya Dkt. Biteko

Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amesema vituo vya kujiandikisha vipo kila kitongoji na kwamba vituo hivyo vinafunguliwa kuanzia saa mbili asubuhi na kufungwa saa 12 jioni na zoezi hilo litaenda hadi tarehe 20 mwezi huu.

Sauti ya RC

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Bukombe Lutengano Mwalwiba amesema wanatarajia kuandikisha wapiga kura 191,124 na jimbo hilo lambapo kuna jumla ya vituo  348.

Sauti ya msimamizi