Viboko, mamba tishio kwa wakazi wa Geita DC
10 May 2024, 5:18 pm
Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita limeketi Mei 8-9, 2024 katika kikao chake cha kawaida kwaajili ya kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli za serikali ngazi ya kata kwa kipindi cha januari hadi machi 202 ambapo jumla ya kata 37 zimewasilisha taarifa katika baraza hilo.
Na: Kale Chongela – Geita
Wanyama wakali aina ya viboko na mamba waendelea kuzua taharuki katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita hasa katika maeneo ya kata ya Nkome, kata ya Nyamboge pamoja na kata ya Butundwe ambapo Wananchi wamekuwa wakishambuliwa na wanyama hao.
Wakitolea ufafanuzi juu ya kero hiyo, baadhi ya Madiwani kutoka katika kata hizo akiwemo Diwani wa kata ya Nkome Masumbuko Sembe amesema hivi karibuni mwananchi mmoja katika eneo lake alivamiwa na wanyama hao hadi kuuawa jambo ambalo liliteta taharuki katika maeneo yao huku wakiitaka idara ya maliasili kuchukulia suala hilo kwa unyeti zaidi.
Afisa maliasili wilaya ya Geita Asaph Manya amewataka madiwani walio katika maeneo hatarishi kutoa taarifa hizo kwa maafisa watendaji wa kata na vijiji na kutoa taarifa kwa Mamlaka husika kwaajili ya kuchanganua changamoto hiz huku akieleza hajawahi kupokea taarifa yoyote mbaya juu ya wanyama hao hatarishi.