Wananchi washirikiana kuziba chanzo cha mafuriko
13 April 2024, 2:35 am
Uduni wa miundombinu ya barabara imekuwa ikichangia athari mbalimbali ambazo zimekuwa zikisababishwa na mvua inayoendelea kunyesha mkoani Geita
Na Kale Chongela – Geita
Baada ya mafuriko kuikumba mitaa mbalimbali ya mkoa geita kutokana na mvua iliyonyesha siku ya April 7, 2024 na kusababisha changamoto kwa wakazi wa mtaa wa Mbugani kata ya kalangalala halmashauri ya mji wa geita.
Hali hiyo imewalazimu baadhi ya wakazi wa mtaa huo wa Mbugani kushirikiana kwa pamoja kuziba eneo ambalo lilikuwa linapitisha maji kutoka katika mtaro unaopitisha maji katika eneo hilo, mtaro uliopasuka kutokana na kuelemewa na maji hivyo kusababisha athari hiyo.
Wananchi hao wakiwa eneo hilo wamebainisha kuwa mtaro huo umekuwa ukipitisha maji ambayo yanatirirrika wakati mvua ikinyesha hali ambayo imekuwa ikipelekea maji kutapakaa kwenye makazi ya watu wa eneo hilo.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya kalangalala Bw. Prudence Temba ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa eneo hilo kwa kujitolea huku akiwataka wananchi wengine wa kata hiyo kujitolea kwenye shughuli za kijamii.