Watoto wajengwe katika misingi ya imani
5 April 2024, 5:04 pm
Mwezi mtukufu wa ramadhani umekuwa chachu ya kujenga jamii katika nyanja mbalimbali ikiwemo amani ,umoja na mshikamano.
Na Mrisho Sadick – Geita
Wanawake Mkoani Geita wametakiwa kutumia kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani kuwajenga watoto wao katika misingi ya kiimani ili kuandaa kizazi chenye hofu ya Mungu.
Kauli hiyo imetolewa na kaimu shekhe Mkuu wa Mkoa wa Geita Mbaraka Mbaraka katika iftari ya wanawake na watoto wanaoishi katika Mazingira magumu iliyoandaliwa na Kikundi cha Wanawake na Samia mjini Geita ambapo amesema kiongozi bora ni yule aliyepata malezi bora namwenye hofu ya Mungu huku akisisitiza wananchi kuendelea kuwa na umoja.
Katibu wa itikadi uenezi na mafunzo wa CCM Mkoa wa Andrew Mnunke Geita amewataka viongozi wa dini na watanzania kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili awatumikie kwa misingi ya utawala bora.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake na Samia Mkoani Geita Adelina Kabakama ameitaka jamii kuacha kubaguana nabadala yake wapendane.