Storm FM
Waziri Jafo aipongeza GGML kwa kuendelea kutunza mazingira
26 September 2023, 7:05 pm
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na meneja wa TFS miti 400 imepandwa katika viwanja vya EPZA Bombambili na Mhe. Jafo.
Na Kale Chongela- Geita
Waziri Wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na Mazingiara Mhe. Selemani Jafo ameipongeza GGML Kwa kuendelea kutunza mazingira kwa kiwango kikubwa .
Mhe. Jafo amesema hayo akiwa katika uwanja Wa EPZ ambapo ndipo yalipo maonesho ya sita ya kimataifa ya Madini mjini Geita.
Akiwa katika banda la GGML amesema Mgodi huo umekuwa chachu kubwa katika suala la utunzaji wa mazingira huku akisisitiza wananchi kupanda miti.