Nuru FM

Waziri Kapinga: Serikali kuendelea kuwajengea uwezo wanawake kiuchumi

28 November 2026, 09:07

Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga akiwa katika kongamano la wanawake Mkoani Iringa. Picha na Adelphina Kutika

Na Adelphina Kutika

Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, amesema Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake wajasiriamali na wafanyabiashara kwa kuwawezesha kupata mitaji na fursa zitakazosaidia kukuza biashara zao na kuzifanya ziwe endelevu.

Kapinga ameyasema hayo katika Kongamano la Wanawake lililofanyika mkoani Iringa, lililolenga kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu fursa mbalimbali za kiuchumi zinazoweza kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji na biashara.

Sauti ya Waziri Kapinga

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amesema pamoja na wanawake kujikita katika shughuli za kiuchumi, wanapaswa pia kuzingatia malezi bora ya watoto, akisisitiza kuwa jukumu la malezi si la mzazi mmoja pekee bali linahitaji ushirikiano wa familia na jamii kwa ujumla.

Sauti ya Kheri

Naye mwandaaji wa kongamano hilo, Dkt. Tumaini Msowoya, amesema kongamano hilo ni jukwaa muhimu la kuwaunganisha wanawake, kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto zinazowakabili katika shughuli zao za kijamii na kiuchumi.

Sauti ya Msowoya

Kongamano hilo limekuwa fursa kwa wanawake kujifunza, kuunganishwa na fursa mbalimbali pamoja na kujadili mikakati ya kukuza shughuli zao za kiuchumi na kujikwamua kimaisha.