Nuru FM
Nuru FM
23 April 2026, 08:49

Mikopo ya Kausha Damu imepelekea wanawake kukimbia ndoa zao
Na Fredrick Siwale
Wananchi Halmashauri ya Mji wa Mafinga wamelalamikia kitendo vya taasisi zinazotoa mikopo kuwafuata na kuwafanyia fujo pale wanapofuata marejesho jambo linalowavunjia utu huku wengine wakiiishi kama wakimbizi.
Wakizungumza na nuru fm baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa licha ya wao kukopa fedha katika taasisi hizo kwa maelewano, bado maafisa wa taasisi hizo wanashindwa kuwadai kwa staha huku wakifika nyakati za usiku kuwatafuta wadaiwa.
Aidha wanachi hao wameiomba serikali kuingilia kati kwa kuziiita Taasisi zilizowakopesha fedha ili wajue namna ya kulipa kwani jambo hilo limepelekea baadhi ya wanawake kukimbia ndoa zao.
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Ivambinungu Uliopo Halmashauri ya Mji Mafinga Bw. Isaack Kikawa amesema kuwa ni kweli wanawake wamekuwa wakikopa fedha Bila kuwashirikisha waume zao jambo lililopeleka ndoa kuvunjika.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Boma Baraka kisakanike amezitaka taasisi zinazokopesha fedha kutumia kfuata haki za msingi pale wanapofuata marejesho yao na kuacha kuwadhalilisha wakopaji.