Nuru FM

Vishoka,Wafanyakazi TRA Watiwa Mbaroni

21 February 2023, 11:24 am

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa habari kuhusu matukio mbalimbali yaliyotokea mkoa wa Iringa

Hii ni baada ya kupokea taarifa na kuunda timu ya upelelezi ambayo ndiyo imefanikisha kuwakamata watuhumiwa hao ambao wamekuwa wakishirikiana na watumishi wa TRA.

Na Hawa Mohammed.

Jeshi la polisi mkoa wa Iringa linawashikilia watu watano wakiwemo watumishi wawili wa TRA kwa kosa la kutoa leseni na kuwapa wananchi bila kufuata  utaratibu.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi amesema kuwa Jeshi la polisi liliwakamata Omary Kibao miaka 38,Johnson Kihongosi miaka 31 na Dikson Nelson miaka 32, ambao wamekiri kushirikiana na  watumishi hao wa TRA kujipatia leseni na namba bila kufuata mfumo uliowekwa kisheria, amesema upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiwabainisha watuhumiwa waliokamatwa

Aidha kamanda ACP Bukumbi amesema watuhumiwa hao walikutwa na namba za magari na pikipiki 431,TIN numbers 08 printer 5, laptop 1, deskitop 1, nakala za vyeti vya mafunzo ya udereva 02, scanner 1 na lamination mashine 1,leseni za udereva 31,kadi za magari 14 pamoja na vitambulisho vya Nida na mpiga kura 04, nakala za gari mbalimbali na police loss report.

Hata hivyo Bukumbi ametoa wito wa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi katika kutoa taarifa kwa wakati zinazohusu viashiria vya uhalifu na wahalifu wakati wote.

Katika hatua nyingine  kamanda Bukumbi amesema Jeshi la polisi linamshikilia mwanamke mmoja anaefahamika kwa jina la Ashura  Hamis aliekutwa akiwa na mafuta aina ya dizeli lita 480 yakiwa kwenye stoo nyumbani kwake

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akielezea kuhusu mtuhumiwa huyo