Nuru FM

Wazee wa Kimila washirikiana na wataalamu wa afya kuhamasisha chanjo ya Uviko-19 Iringa

3 April 2023, 2:57 pm

Viongozi wa Kimila Mkoani Iringa wametajwa kuwa sababu ya wananchi kujitokeza kupata chanzo ya Uviko-19.

Na Ashura Godwin

Wananchi Mkoani Iringa wameanza kuwa na  mwamko wa kupata chanjo ya uviko-19 baada ya kupata elimu na hamasa kutoka kwa viongozi wa kimila kwa kushirikiana na wataalamu wa afya.

Hayo yamezungumzwa na mratibu wa chanjo Mkoa wa Iringa Hansi mapunda  na kuongeza kuwa kuna na mwamko mkubwa kwa jamii kufanya maamuzi ya kupata chanjo ya uviko -19 kupitia hamasa za viongozi hao kutokana na imani wakizokuwa nazo katika jamii zao.

“Kwa kweli viongozi wa Dini wamekuwa na mchango mkubwa sana wa kuhanmasisha wananchi kujitokeza kupata chanjo ya Uviko-19” alisema Mapunda

Gerald Malangalila ni Kongozi wa kimila Mkoa wa Iringa amesema wamekuwa wakishirikishwa na idara za afya kuhamasisha chanjo jambo ambalo limepeekea wananchi wao kufanya maamuzi ya kuchanja.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya iringa VERONIKA KESSY  amewasisitiza viongozi wa kimila kuendelea kutoa ushirikiano katika kuhamisha wananchi wanapata chanjo ya uviko -19.

Nao baadhi ya wananchi Manispaa ya Iringa wamesema kuna umuhimu mkubwa wa viongozi wa kimilila kuendelea kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa chanjo ya uviko -19 kutokana na nguvu kubwa walionayo katika jamii.

MWISHO