Nuru FM

Samia, Chongolo wazawadiwa ng’ombe Mufindi Kusini

29 May 2023, 5:52 pm

Mbunge wa Mufindi Kusini David kihenzile mwenye microphone akikabidhi ng’ombe kwa Katibu Mkuu CCM Taifa. Picha na Kyamba.

Na Mwandishi wetu

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti Wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania David Kihenzile amekabidhi zawadi ya ng’ombe kwa ajili ya Mh.Rais Samia Suluhu Hassan.

Hata hivyo amekabidhi pia ng’ombe wa pili kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Daniel Chongolo.

Katibu Mkuu Chongolo amepokea ng’ombe hao kwenye mkutano uliofanyika wilaya ya Mufindi kata ya Nyololo ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi CCM mkoani Iringa.

Ng’ombe aliyekabidhiwa kwa Katibu Mkuu CCM Comred Daniel Chongolo

Akizungumza baada ya kukabidhi ng’ombe hao, Mh. Kihenzile amesema kuwa anashukuru kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika jimbo la Mufindi Kusini hasa ikiwemo ujenzi wa majengo mapya ya madarasa sambamba na ukarabati katika shule za msingi na sekondari, ujenzi wa hosptali ya wilaya, ujenzi wa barabara za lami, sambamba na uboreshwaji wa barabara zilizokuwa zimechakaa pia kuboresha sekta ya maji pamoja na nishati ya umeme kwa baadhi ya vijiji vilivyopo jimboni hapo.

“Zawadi hizi zimetolewa na Wanamufindi Kusini na mimi ninazikabidhi kwa niaba ya kuwawakilisha wananchi wa Mufindi Kusini kadhalika wamenituma niwasilishe salamu nyingi kwa Rais Samia na pongezi kwa kazi kubwa na nzuri zenye msingi wa kujenga na kubolesha taifa bora” Alisema Kihenzile