Nuru FM

Wafanyakazi Nuru FM wapigwa msasa uandishi wenye tija

30 April 2024, 10:38 am

Wafanyakazi wa Radio Nuru FM wakifuatilia Mafunzo yaliyotolewa na Hillali Ruhundwa kutoka TADIO. Picha na Hafidh Ally

Waandishi wa habari Radio Nuru FM wameaswa kufuata weledi katika uandishi wa habari.

Na Hafidh Ally

Wafanyakazi wa Nuru FM radio iliyopo Mkoani Iringa wamepatiwa Mafunzo ya namna ya kuandaa maudhui na kuchapisha katika Mtandao wa Radio Tadio.

Akizungumzia kuhusu Mafunzo hayo, Mkufunzi kutoka Mtandao wa Radio jamii Tanzania -TADIO- Bw. Hillali Ruhundwa amesema kuwa ni vyema wafanyakazi hao wakajikita katika kuandaa maudhui na kufuata weledi na maadili ya uandishi wa habari.

“Pindi mnapoandaa maudhui haya mnatakiwa mfuate miiko ya uandishi wa habari ili kupunguza makosa yanayojitokeza katika uandaaji” Alisema Hillali

Aidha amesema kuwa ili kuongeza idadi ya wafuatuliaji wa Mtandao huo ni vyema wafanyakazi hao wakawa na Utaratibu wa kusambaza maudhui hayo katika mitandao ya kijamii.

Kwa upande wake Mhariri Mkuu wa Radio Nuru FM Hafidh Ally amesema kuwa watahakikisha wanafanyia kazi kwa Vitendo Mafunzo hayo ili waweze kuandaa maudhui yanayowahusu wananchi wanaowazunguka.