Nuru FM

Mnec Asas apongezwa na Mbunge Kabati kwa kishiriki Miradi ya Maendeleo Iringa

17 April 2023, 5:00 pm

Mbunge Kabati akitoa pongezi kwa MNEC ASAS kushiriki shughuli za kimaendeleo. Picha na Hafidh Ally

Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Mkoa wa Iringa MNEC Salim Asas amekuwa akishiriki katika shughuli za miradi ya kimaendeleo Mkoani Iringa jambo ambalo linapaswa kuigwa na wadau wengine.

Na Hafidh Ally

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati amempongeza Mnec Salim Asas kwa kujitoa katika miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wa Iringa.

Ritta kabati ametoa Pongezi hizo Bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akichangia Hoja katika Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI na kuongeza kuwa ni vyema serikali ikawakumbuka wadau hao akiwemo ASAS ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wakazi wa iringa wanakuwa kiustawi, kiuchumi na kijamii.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Ccm Taifa- MNEC Salim Asas wakifuatilia jambo katika shughuli za Chama chao.
Sauti ya Kabati

Amesema kuwa Mnec ASAS ameshiriki katika miradi mingi ikiwemo ujenzi wa jengo la Damu salam, jengo la viungo bandia, jengo la wagonjwa maalumu (VIP), Kuchangia Shilingi Milion 100 kwa ajili ya ujenzi wa vibanda vya wamachinga.

Hata hivyo Kabati amebainisha kuwa miradi mingine ambayo Asas ameshiriki ni pamoja na ujenzi wa jengo la ustawi wa Jamii ambalo waziri mkuu alifika na kulingua, Jengo la ICU, huku akiwaomba wabunge wapitishe Azimio la Kuwapongeza wadau wote ambao wanaisaidia serikali kutekeleza miradi ya kimaendeleo.

MWISHO