Nuru FM

Wizara ya Maji Yaikumbuka Ilalasimba

17 February 2023, 4:19 pm

Ujenzi wa mradi huo wa bwawa la Ilalasimba katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa uliofanyiwa upembuzi yakinifu tangu mwaka 2018 sasa watarajiwa kujengwa.

Na Hawa Mohammed.

Zaidi ya shilingi bilioni mbili (2) zimetengwa na Wizara ya maji kwa ajili ya ujenzi wa Bwawa maalum kwa  shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo cha umwagiliaji na ufugaji samaki katika kijijji cha Ilalasimba kata ya Nzihi Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Steven Mhapa amewaondoa hofu wakazi wa kijijji hicho  kutokana na kuchelewa kwa ujenzi wa mradi huo wa kiuchumi uliofanyiwa upembuzi yakinifu tangu mwaka 2018.  

Mhapa akiwataka wananchi katika kijiji hicho kuondoa hofu kuhusiana na ujenzi wa Bwawa hilo

Aidha Mhapa amesema ujenzi wa bwawa hilo litaongeza mapato ya kijiji hicho na wananchi kwa ujumla kutokana na shughuli zinazotarajiwa kufanyika.

Mhapa akieleza namna Bwawa hilo litakavyokuza uchumi kwa wananchi na kijiji

Awali wananchi wa kijiji cha Ilalasimba wamesema walizuiwa kufanya shughuli zao ikiwemo kilimo katika eneo hilo kwa kipindi kirefu hali inayorudisha  nyuma shughuli za kimaendeleo kwa kuwa hakuna ujenzi unaoendelea na kwamba wanaamini suala hilo linakwamishwa na siasa.

Wananchi wa kijiji cha Illalasimba wameeleza kukwama kwa ujenzi wa Bwawa hilo kulivyowakwamisha kiuchumi