Nuru FM

Wananchi Kiwele waomba josho la kuogeshea mifugo

26 April 2024, 9:58 am

Josho la kuogeshea mifugo. Picha kwa msaada wa mtandao

Kuogesha mifugo ni muhimu sana kwani husaidia katika kudhibiti wadudu wanaosababisha magonjwa.

Na Joyce Buganda

Wananchi wa kata ya Kiwele iliyopo jimbo la Kalenga  mkoani  Iringa wanakumbana na changamoto ya ukosefu wa josho jambo linalopelekea kutembea umbali mrefu kwenda kuogesha mifugo yao.

Wakizungumza na kituo hiki  baadhi ya wananchi hao wamesema kuwa toka wameahidiwa kuwepo na josho la kuogesha mifugo yao imepita miaka mine huku wakienda katika kijiji cha Kiwele kufuata josho.

Sauti ya Wananchi

Kwa upande wa Mwenyekiti wa kijiji cha Mfyome Richard Luhala amesema kuwa kijiji cha Mfyome na Itagutwa vina idadi kubwa ya mifugo hivyo josho likiwepo katika vijiji hivyo itapunguza usafirishaji wa mifugo na kuzuia mmomonyoko wa ardhi.

Sauti ya Mwenyekiti Mfyome

Naye Diwani wa kata ya Kiwele Felix Waya  amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na ameeleza kuwa endapo josho litapatikana kati ya kijiji cha itangutwa na mfyome itawapunguzia adha wafugaji ya kutembea kilomita 20 kupeleka mifugo kuogesha katika majosho jirani.

Sauti ya Diwani