Nuru FM

Mh. Kiswaga akabidhi viti 10 Tagamenda

31 October 2021, 7:01 pm

Mbunge wa Jimbo la Kalenga Mh. Jackson Kiswaga amekabidhi Viti 10 vya plastiki katika kijiji cha Tagamenda baada ya kuahidi katika ziara zake za kikazi.

Mh. Kiswaga ametoa viti hivyo mara baada ya kutembelea kijiji hicho na kukabidhi kwa mwenyekiti wa kijiji hicho cha Tagamenda Bw. Job Mbuza na kuongeza kuwa huo ulikuwa ni uhitaji wa kijiji hicho.

Aidha Mh. Kiswaga amebainisha kuwa huo ni utekekezaji wa ahadi zake mara baada ya uongozi wa kijiji hicho kumuomba viti 10 kutokana na ukosefu wake huku akiwataka kuendelea kuwatumikia wananchi wao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Tagamenda  Job Mpunza amekiri kupokea viti hivyo huku akimpongeza Mbunge Kiswaga kwa kutekeleza ahadi yake ambayo aliitoa katika mkutano wa kijiji chao.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake Mkazi wa Tagamenda Bw. Isihaka Mbata amempongeza Mbunge Jackson Kiswaga kwa kutekeleza ahadi hizo ikiwemo kuwatembelea wananchi wa jimbo hilo kwani ameonesha mfano katika kipindi kifupi cha utawala wake.

Mwezi wa Tisa Mwaka huu Mh. Kiswaga aliombwa viti 10 na wananchi wa kijiji cha Tagamenda baada ya kuwa na ofisi ya kijiji huku wakikabiliwa na changamoto ya viti ambayo tayari ameshaitatua.

MWISHO