Nuru FM

Madaktari bingwa kutoka JKCI kuweka kambi Iringa

16 April 2024, 10:09 am

Dkt. Pedro Pallangyo Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na mkuu wa idara ya tafiti ,mafunzo na upimaji afya kwa jamii kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI. Picha Adelphina Kutika

Serikali imefanya jitihada za kukabiliana na Magonjwa yasiyoambukiza kwa kuwaleta wataalamu kutoka Taasisi ya JKCI Mkoani Iringa kuweka Kambi ya kuwahudumia wakazi wa Mkoa huu.

Na Adelphina Kutika

MAMIA ya Wananchi kutoka maeneo mbalimbali mkoani Iringa  wamejitokeza kwa wingi kwenye kambi ya Huduma za Madaktari Bingwa kwa Uchunguzi wa magonjwa moyo  kutoka taasisi ya  moyo   (JKCI) .

Akizungumza na vyombo vya habari Dr Scholastica Malangalila Kaimu Mganga Mfawidhi Iringa amesema Kambi hiyo ya Huduma za Madaktari Bingwa  wa Moyo  itadumu siku tano ambapo siku ya kwanza ya zoezi hilo mwitikio wa wananchi walijitokeza  ni takribani  wananchi 120 lengo ni  kuwafikia  wagonjwa  zaidi ya 800.

Sauti ya Dr. Scholastica

Dkt. Pedro Pallangyo Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo na mkuu wa idara ya tafiti ,mafunzo na upimaji afya kwa jamii kutoka Taasisi ya Magonjwa ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI  amesema dawa za kuongeza nguvu na nishati zimekuwa zikiathiri mfumo wa binadamu kufanya kazi hali inayopelekea kupanda kwa presha ,kiharusi na moyo kusimama ghafla .

Sauti ya Dr Pedro

Kwa upande wao baadhi ya  wa wananchi hao frank na anna  wamesema kwamba ujio wa huduma hiyo  umekuja wakati muafaka kwani hivi sasa wananchi wengi wamekuwa  wakitumia gharama kubwa kufuata  matibabu hivyo wanaiomba serikali kuwe na utaratibu wa mara kwa mara kwa clinic hizo.

Sauti ya wananchi Iringa