Nuru FM

Mradi wa USAIDS Kizazi Hodari wawafikia watoto 9000 Iringa na Njombe.

14 November 2023, 4:12 pm

Mkurugenzi Wa Mradi Huo Doroth Matoyo akizungumza na Wanahabari. Picha na Denis Nyali.

Na Denis Nyali

Jumla Ya Watoto 9000  Walioambukizwa Virusi Vya Ukimwi Wamefikiwa Na Mradi Wa USAIDS Kizazi Hodari Unaotelelezwa Kwa Mkoa Wa Iringa Na Njombe Na Kuwaunganisha Na Vikundi Mbalimbali Katika Kuwawezesha Kupata Kiuchumi.

Akizungumza  Na Nuru Fm Mkurugenzi Wa Mradi Huo Doroth Matoyo Amesema  Mradi Huo Unaofanya Kazi Ya Kuwasaidia Watoto Walioambukizwa Virusi Vya Ukimwi Na Kuwaunganisha  Watoto Kwa Taassisi Za Dini Pamoja Na Vituo Vya Lishe Ili Kuwawezesha Kutimiza Ndoto Zao Na Kuongeza Kuwa Jumla Ya Watoto 9000 Wamefikiwa Na Mradi Huo.

Bi Matoyo Ameongeza Kuwa Kumekuwa Na Chanagamoto Ya Baadhi Ya Watoto  Kutoikubali Hali Ambapo Wao Kama Mradi Wamekuwa Na Utaratibu Wa Kuwaunganisha Na Wafanyakazi Wa Ngazi Ya Jamii Pamoja Na Wataalamu Wa Afya Pamoja Na Wanasaikolojia.

Katika Kukabiliana Na Changomoto Za Kiuchumi Na Kuwawezesha Kujitegemea Mradi Umewaunganisha Wazazi Na  Walezi Katika Vikundi Vya Kukopa Vya Halamashauri  Kupata Mikopo Ya Wanawake Kupitia Vikundi Mbalimbali  Ili Kuwawezesha Kiuchumi.