Nuru FM

Watalaam wa afya toka hospitali ya Rufaa Iringa watoa msaada kituo cha IOP

10 June 2023, 7:28 am

Madaktari na wataalam kutoka Hospital ya Rufaa Iringa wakisikiliza jambo katika kituo cha IOP. Picha na Ansigary Kimendo.

Na Ansigary Kimendo

Madaktari na wataalam mbalimbali wa afya kutoka hospitali ya rufaa mkoa wa Iringa, wametembelea kituo cha kulea watoto yatima cha Ilula Orphan Program (IOP) na kutoa mahitaji mbalimbali ikiwemo Chakula.

Wamesema lengo ni kuifikia jamii yenye uhitaji na zoezi hilo ni endelevu ambapo baada ya kutembelea kituo hicho watafika kwenye maeneo mengine yenye uhitaji.

Baadhi ya madaktari waliotembelea kituo cha IOP wakipata maelekezo kutoka mwenyeji wao Ajolom Mgeveke.

“Sisi tutahakikisha tunawafikia watu wenye uhitaji ili na wao wapate mahitaji ambayo tumewaandalia” Walisema madaktari hao

Mbali na kutoa misaada, madaktari hao wameweza kucheza mechi ya hisani dhidi ya wasimamizi wa kituo hicho ambapo mchezo umemalizika kwa sare ya 1-1.