Nuru FM

Shirika la ndege la KLM laiomba Radhi Tanzania

30 January 2023, 7:00 am

Shirika la ndege la KLM limetoa ufafanuzi na kuomba radhi juu ya kusitisha safari zake za ndege kuja Tanzania pamoja na kutoa taarifa ya uwepo wa machafuko Nchini.

Kupitia barua ya Meneja wa Air France-KLM Tanzania, kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa KLM imesema:-

“Tunasikitika hatukueleza sababu iliyotufanya tuamue kusitisha safari za ndege zetu Dar es Salaam kwa sasa kwa usahihi. Matumizi ya kauli ‘machafuko ya kiraia’ hayakuwa sahihi, ambayo tunaomba radhi kwa kauli hiyo.

Ndege ya shirika la KLM

“Tishio maalum la ndani limetusukuma kufanya uamuzi huu. Hatuwezi kutoa maelezo zaidi kuhusu suala hili la usalama. Tulizingatia maoni yako na tumerekebisha ujumbe kwenye tovuti yetu.”

“Tunashughulikia mchakato wa kuanzisha upya safari za ndege za Dar es Salaam, Kilimanjaro na Zanzibar haraka iwezekanavyo. Hili linahitaji marekebisho ya kiutendaji ili kuwafanya wafanyakazi wetu kutua nje ya Dar es Salaam.”