Nuru FM

Kabati aipongeza serikali kwa kuandaa mazingira mazuri mikopo 10%

30 May 2023, 9:35 am

Kabati akizungumza katika kongamano la wanawake wajane. Picha na Mwandishi wetu

Na Hafidh Ally

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati ameipongeza serikali kwa kuweka mkakati madhubuti wa utoaji fedha asilimia 10 katika halmashauri nchini.

Kabati ametoa pongezi hizo katika kongamano la wajane wa mkoa wa Iringa lililoandaliwa na Kanisa la Kilutheri Tanzania KKKT mkoa wa Iringa na kukutanisha zaidi ya wanawake wajane 1500.

Dkt. Kabati amesema serikali ya mama Samia imesitisha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili kuweka utaratibu mzuri wa wanawake wote nchini kufaidika na mikopo hiyo.

Amesema kuwa ni muda muafaka sasa kwa kundi hilo kuandaa mazingira rafiki yatakayopelekea kupata fedha hizo ili waweze kujiinua kiuchumi.

Katika hatua nyingine Kabati amesema serikali ya awamu ya sita ya mama Samia Suluhu Hassan imetenga fedha kwa ajili msaada wa kisheria wa wanawake wajane wanaopata shida katika mirathi.

MWISHO