Nuru FM

Rais Samia awafagilia mawaziri vijana

8 June 2022, 3:18 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Jumatano (Juni 08) ameanza ziara ya kikazi mkoani Kagera, kwa kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Buharamuro.

Rais Samia alisismama wilayani humo akiwa safarini kuelekea Wilaya ya Bukoba Mjini akiambatana na baadhi ya Mawaziri wake, ambao pia walipata nafasi ya kuzungumza na wananchi wa Biharamuro na kueleza namna walivyotatua shida zao.

Rais Samia amekiria kuridhishwa na utendaji kazi wa mawaziri hao, huku akiwataka Wananchi kuendelea kushirikiana na mawaziri wake, ili kutatua kero zinazowasilishwa na wawakilishi wao Bungeni, na kwenye mabaraza ya Madiwani nchini kote.

“Hawa ndiyo mawaziri wenu Vijana na wapo hapo ili waweze kuwahudumia ninyi wananchi na niliwachagua wa mawaziri hawa, ili wanapokosea niwaadhibu na wengine ni wenyeji wa huku, ni watoto wenu hivyo wapo nyumbani,” amesema Rais Samia.

Awali akimkaribisha Rais Mkoani humo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Bi. Constansia Buhiye, alisema kwa mara ya kwanza Samia Suluhu Hassan amefika mkoani humo akiwa kama Rais na kumpongeza kwa kazi nyingi anazozifanyahuku akimtaka asimame imara ili kufikia malengo ya nchi.