Maazimio 15 yawekwa kati ya wanahabari, polisi Iringa
18 March 2024, 11:23

Maazimio 15 yamefikiwa kuelekea kwenye chaguzi za serikali za mitaa ili kuongeza ushirikiano kati ya Polisi na Wanahabari.
Na Mwandishi wetu.
Jeshi la Polisi na waandishi wa habari mkoani Iringa wameweka maazimio 15 yatakayowaongoza kufanya kazi na kujenga uwezo wa kiusalama na kiulinzi kati ya waandishi wa habari na jeshi la polisi mkoa wa Iringa.
Hayo yamejiri baada ya kukamilika kwa midahalo minne ya ulinzi na usalama wa waandishi wa habari, ambayo imedhaminiwa na 𝐔𝐦𝐨𝐣𝐚 𝐰𝐚 𝐊𝐥𝐚𝐛𝐮 𝐳𝐚 𝐖𝐚𝐚𝐧𝐝𝐢𝐬𝐡𝐢 𝐰𝐚 𝐇𝐚𝐛𝐚𝐫𝐢 𝐓𝐚𝐧𝐳𝐚𝐧𝐢𝐚 (𝐔𝐓𝐏𝐂) 𝐤𝐮𝐩𝐢𝐭𝐢𝐚 𝐒𝐡𝐢𝐫𝐢𝐤𝐚 𝐥𝐚 𝐊𝐢𝐦𝐚𝐭𝐚𝐢𝐟𝐚 𝐥𝐚 𝐊𝐮𝐬𝐚𝐢𝐝𝐢𝐚 𝐕𝐲𝐨m𝐛𝐨 𝐯𝐲𝐚 𝐇𝐚𝐛𝐚𝐫𝐢 (𝐈𝐌𝐒) lenye lengo la kujenga uwezo wa kiusalama na kiulinzi kwa waandishi wa habari.
Akizungumza katika utiliwaji wa saini wa maazimio hayo, 𝐌𝐰𝐞𝐧𝐲𝐞𝐤𝐢𝐭𝐢 𝐰𝐚 𝐖𝐚𝐚𝐧𝐝𝐢𝐬𝐡𝐢 𝐰𝐚 𝐇𝐚𝐛𝐚𝐫𝐢 𝐌𝐤𝐨𝐚 𝐰𝐚 𝐈𝐫𝐢𝐧𝐠𝐚 𝐍𝐝𝐮𝐠𝐮 𝐅𝐫𝐚𝐧𝐤 𝐋𝐞𝐨𝐧𝐚𝐫𝐝 amesema makubaliano hayo, yakizingatiwa kwa makundi yote mawili, yataleta ufanisi kwa makundi hayo akiwataka waandishi wa habari na jeshi la polisi kuzingatia misingi ya maadili na taaluma ya kazi zao, huku akiwakumbusha waandishi wa habari kwamba hakuna habari kubwa kama maisha yao.
𝐊𝐰𝐚 𝐮𝐩𝐚𝐧𝐝𝐞 𝐰𝐚𝐤𝐞, 𝐊𝐚𝐦𝐚𝐧𝐝𝐚 𝐰𝐚 𝐏𝐨𝐥𝐢𝐬𝐢 𝐌𝐤𝐨𝐚 𝐰𝐚 𝐈𝐫𝐢𝐧𝐠𝐚 𝐒𝐀𝐂𝐏 𝐀𝐥𝐥𝐚𝐧 𝐋. 𝐁𝐮𝐤𝐮𝐦𝐛𝐢 amesema makubaliano hayo ni muhimu hasa tunapoelekea kwenye chaguzi za serikali za mitaa huku akitoa rai kwa makundi yote mawili kuzingatia makubaliano hayo ili kufikia lengo la mashikiano hayo.
𝐊𝐚𝐭𝐢𝐛𝐮 𝐰𝐚 𝐖𝐚𝐚𝐧𝐝𝐢𝐬𝐡𝐢 𝐰𝐚 𝐇𝐚𝐛𝐚𝐫𝐢 𝐌𝐤𝐨𝐚 𝐰𝐚 𝐈𝐫𝐢𝐧𝐠𝐚 𝐍𝐝𝐮𝐠𝐮 𝐇𝐚𝐤𝐢𝐦𝐮 𝐌𝐰𝐚𝐟𝐨𝐧𝐠𝐨 𝐚𝐦𝐞𝐬𝐨𝐦𝐚 𝐦𝐚𝐚𝐳𝐢𝐦𝐢𝐨 𝐡𝐚𝐲𝐨 𝟏𝟓,baadhi yakiwa ni kuimarisha ushirikiano kwa makundi hayo, kufanya tathmini ya pamoja ya makubaliano hayo kila baada ya miezi mitatu, UTPC na wadau wengine kuendelea kutoa mafunzo ya ulinzi na usalama na waandishi wa habari kuzingatia usalama wao wanapochukua habari 𝐡𝐮𝐤𝐮 𝐯𝐢𝐨𝐧𝐠𝐨𝐳𝐢 𝐰𝐚 𝐝𝐢𝐧𝐢 𝐧𝐚 𝐰𝐚𝐧𝐚𝐬𝐡𝐞𝐫𝐢𝐚 𝐰𝐚𝐤𝐢𝐬𝐡𝐮𝐡𝐮𝐝𝐢𝐚 𝐦𝐚𝐤𝐮𝐛𝐚𝐥𝐢𝐚𝐧𝐨.