Nuru FM

Mafinga Mji wavuka lengo la ukusanyaji mapato

13 May 2026, 10:14

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga akizungumza katika Baraza la Madiwani. Picha na Fredrick Siwale.

Halmashauri hiyo imefanikiwa kukusanya zaidi ya shilingi Bilion 8.8 na kufanikiwa kuvuka lengo kwa asilimia 105 ya makusanyo ambayo walikadiria kukusanya shilingi Bilion 7.5.

Na Fredrick Siwale

Halmashauri ya Mji mafinga imefanikiwa kuvuka lengo la kukusanya mapato ya ndani kwa asilimia 105 katika kipindi cha robo tatu ya mwaka 2025/2026.

Akizungumza katika cha Kikao cha Baraza la Madiwani Halmshauri ya Mji Mafinga kutoa tathmini ya Robo tatu ya mwaka 2025/2026, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo  Bw. Reginant Kivinge amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na ushirikiano baina ya madiwani na wakuu wa idara kwa kufanya kazi kwa weledi.

Sauti ya Kivinge

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Mafinga, Bi Fidelica Myovella amebainisha kuwa Halmashauri hiyo itazidi kufuata maelekezo ya serikali ikiwemo kujibu hoja na masuala ya ufungaji wa hesabu ili kuendeleza kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato.

Sauti ya Myovella

Naye Afisa Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Sifael Kivamba ameipongeza halmashauri hiyo kwa kuvuka lengo la kusimamia zoezi la ukusanyaji wa mapato ya ndani huku akiwataka kuendeleza mkazo huo katika mwaka ujao wa fedha.

Sauti ya Sifael