Sanga: “Wanamasaka Mtapata huduma bora”
15 May 2026, 15:16

Kituo hicho kitasaidia wananchi hao kupata huduma bora za afya.
Na Joyce Buganda
Wananchi wa Kijiji cha Kaning’ombe kilichopo Kata ya Masaka Wilaya ya Iringa wameiomba serikali kuwajengea kituo cha afya sambamba na kuwatatulia changamoto ya maji.
Wakizungumza katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo, baadhi ya wananchi wamesema kuwa kata hiyo imekuwa na changamoto ya kutokua na kituo cha afya jambo linalopelekea kukosa huduma bora za afya.
Diwani wa Kata ya Masaka Yohanes Sanga amesema kuwa dhamira yake ni kuhakikisha wananchi wa Kata hiyo wanapata huduma bora ikiwemo kuwa na kituo cha afya wakati wakiendelea na mchakato wa kila kijiji kuwa na zahanati.
Aidha Mh. Sanga amebainisha kuwa baada ya kuona kuna mradi mkubwa wa maji ambao utavinufaisha vijiji vya kata hiyo ili kuwasaidia wananchi hao katika kilimo na shughuli nyingine.
Diwani huyo amesema kuwa wataendea kufanya mikutano ili kuwapa wananchi nafasi ya kueleza changamoto zao pamoja na kutafuta suluhisho kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa eneo hilo.