Nuru FM

Mbunge Kabati ajionea kero ya barabara Kilolo

3 March 2026, 10:14

Wananchi wa Kilolo wakizungumzia changamoto ya barabara mbele ya Mbunge Kabati. Picha na Hafidh Ally

“Serikali itahakikisha Barabara zinapitika Kwa Mwaka mzima hasa katika Misimu ya Mvua kwa kuzikarabati” Kabati

Na Hafidh Ally

Wananchi wa Jimbo la Kilolo Mkoani Iringa wamelalamikia changamoto ya ubovu wa barabara za Jimbo hilo hasa njia za Dabaga na idete katika kipindi cha msimu wa mvua.

Wakizungumza mara baada ya Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mh. Ritta Kabati kufanya ziara ya kujionea hali halisi ya miundombinu Ya Barabara hiyo, Wananchi hao wamesema kuwa ni vyema serikali ikaifumua barabara hiyo na kuitengeneza kwa kiwango cha lami.

Sauti ya Wananchi

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Dabaga Mh. Amini Joseph Tengilakwi amesema kuwa barabara ya Dabaga imekuwa changamoto ya muda mrefu ambapo wafanyabiashara wanashindwa kusafirisha mazao yao kutokana na ubovu wa moundombinu ya barabara.

Sauti ya Diwani

Naye Mbunge wa Jimbo la Kilolo Mh. Ritta Kabati amesema kuwa atahakikisha anashirikiana na Tanroad na Tarura kuhakikisha barabara hizo zinapitika wakati wote.

Sauti ya Mbunge Kabati